
| 
   Contact us: 
 AVIC Consultants Plot 60 Block 45, Kajenge Street, Kijitonyama, P O Box 11924, Dar es Salaam, Tanzania 
  | 
 
| 
   SABABU YA KUANZISHA ONLINE TV Kilicho sababisha wamiliki wa Tan Business Channel kuanzisha Online TV, ni baada ya kutambua kuna changamoto ya ajira, inayo wakabili vijana wetu Vijana wetu wanao hitimu vyuo vikuu na vyuo vya kati, wanakabiliwa na changamoto ya kupata ajira kutoka sekta binafsi na serikalini. Kutokana na hali hiyo, viongozi waTan Business Channel tumeamua kuanzisha Online TV, ili ifundushe elimu ya ujasiriamali kwa vijana wetu. WALENGWA WA VIPINDI VYA TAN BUSINESS ONLINE TV Tan Business Channel Online TV, inatangaza vipindi ambavyo vinakidhi mahitaji ya watazamaji tunao walenga Watamazaji tunao walenga ni vijana wenye umri kati ya miaka 18-35 ambao wanahitaji elimu ya ujasiriamali. Matumaini yetu ni kuwa, elimu ya ujasiriamali watakayopata vijana wetu, itawasaidia kujiajiri wenyewe VIPINDI VYA TAN BUSINESS CHANNEL ONLINE TV Kuna aina 3 za vipindi vinavyo tangazwa na Tan Business Channel kama vifuatavyo: · Kuanzisha biashara · Kusimamia biashara · Kutengeneza hesabu za biashara  | 
 
| 
   KUANZISHA BIASHARA Kipindi cha kuanzisha biashara, ni muhimu kwa kuweka misingi imara, wakati wa kuanzisha biashara 
 Iwapo biashara haitakuwa na misingi imara wakati wa kuanzisha, ni wazi kuwa hiyo biashara haitakuwa endelevu 
 Hali ya kusuasua kwa biashara kama itaendelea, kuna uwezakano mkubwa wa biashara kufilisika KIPINDI CHA KUENDELEZA BIASHARA Iwapo unafakiwa kuweka misingi imara ya biashara mpya, ni muhimu kufanikisha kuwa na biashara endelevu 
 Unaweza kuwa na biashara endelevu, kwa kuweka mfumo mzuri wa kusimamia biashara. Huo mfumo unatakiwa kufanikisha biashara kufanyika kwa ufanisi na faida inapatikana KUTENGENEZA HESABU ZA BIASHARA Huwezi kufanikiwa kuwa na biashara endelevu kama hutengenezi plan ya biashara na kufuatilia utekelezaji wake 
 Kupima ufanisi wa utekelezaji wa plan za biashara, kunahitaji utengenezaji wa taarifa za biashara 
 Moja ya taarifa za biashara ambayo ni ya muhimu, ni ya hesabu za biashara. Taarifa ya hesabu za biashara inaeleza mambo muhimu yafuatayo: · Kama biashara inapata faida au hasara · Kama kuna mtiririko mzuri au mbaya wa fedha za biashara · Kama kuna ongezeko au upungufu wa mali, madeni, faida na mtaji wa biashara  | 
 

| 
   Usikose kuangalia kipindi cha Dira ya Ujasiriamali siku za Jumatatu-Jumamosi 9.00-10.00 PM 
 https://youtube.com/alimwambola 
  | 
 
| 
   Pata elimu ya ujasiriamali kupitia Tan Business Online School 
  | 
 
| 
   TAN BUSINESS CHANNEL ONLINE TV  | 
 
| 
   TAN BUSINESS BOOK PUBLISHING  | 
 
| 
   TAN BUSINESS ONLINE SCHOOL  | 
 
| 
   Tan Business Channel  |